Breaking News

Waaswa kutumia vituo vya kilimo na ufagaji ili kuongeza uzalishaji.

WAKAZI wa mkoa wa Rukwa, wametakiwa kujenga utamaduni wa kutembelea kituo cha rasilimali za kilimo na mifugo ili kupata ushauri utakaowawezesha kutumia teknolojia bora za uzalishaji wa mazao na mifugo hali ambayo itasaidia kuongeza tija na uzalishaji wa mazao yao.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Willium Shimwela akikata utepe ikwa ni ishara ya kuzindua kituo cha rasilimali za kilimo na mifugo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoa humo, Willium Shimwela
alisema hayo mara baada ya kuzindua kituo cha kisasa cha rasilimali za kilimo na mifugo kilichopo kwenye katika kijiji cha Katumba Azimio kwenye kata ya Pito nje kidogo ya manispaa hiyo.

Shimwela alisema kuwa iwapo wakulima watatumia fursa ya uwepo wa kituo hicho ili kupataa taarifa za mbalimbali na ushauri wa matumizi ya teknolojia bora za uzalishaji wa mazao na mifugo wataweze kuongeza tija na uzalishaji hali ambayo itasaidia kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi hao.
 Afisa Mifugo wa Manispaa ya Sumbawanga, Peter Mtalimbo akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,  kuhusu vifaa vinavyotumika kwa vitendo kuelimisha wananchi kuhusu ufugaji wa kisasa.

Awali, Afisa Kilimo, umwagiliaji na ushirika, George Lupilya alisema kuwa kituo hicho kitatumika si tu kutoa elimu pekee kwa wakulima na wafugaji lakini pia kufanya utafiti wa mbegu bora ili waweze kutumia mbegu bora na za kisasa zitakazowasaidia kuzalisha mazao kwa kiwango cha juu.
                      Afisa Kilimo, umwagiliaji na ushirika, George Lupilya, akisoma taarifa ya kituo hicho.

Alisema kuwa pia suala la kuwatafutia masoko wakulima litafanywa kwenye kituo hicho kwa kuwa ni kitovu cha habari hivyo  taarifa zote za bei ya mazao hususani mahindi ndani na nje ya nchi zitakuwa zikipatikana katika kituo hicho.

"kituo kitatoa huduma za maktaba na mawasiliano na kubadilishana habari za kitaalam kati ya wilaya, mkoa, kanda na hata taifa lengo ni kumsaidia mkulima na mfugaji kupata taarifa zenye kuleta tija katika uzalishaji wake" alisema.

Mshereheshaji wa hafla hiyo, Mr Misasi kutoka ofisi ya katibu tawala mkoa upande wa uchumi na uzalishaji akionyesha mbwembwe zake.

No comments