Breaking News

Wafanyabiashara marufuku kuuza mahindi NFRA

SERIKALI imeiagiza mamlaka ya hifadha ya Chakula ya taifa (NFRA) kuacha kununua mahindi kutoka kwa wafanyabiashara badala yake iwape kipaumbele wakulima ambao ndio walengwa wakubwa wa soko hilo.
Meneja wa mamlaka ya hifadhi ya taifa ya Chakula (NFRA) kanda ya Sumbawanga, Amos Mtafya (Kushoto) akitoa maelezo kuhusu uwezo wa tani ambazo hifadhi hiyo inaweza kuhifadhi mahindi kwa Naibu wa waziri wa kilimo chakula na ushirika Godfrey Zambi alipotembelea kituo cha NFRA Sumbawanga mjini mkoani Rukwa jana, kituo hicho kina uwezo wa kuhifadhi tani 38 tu za mahindi.

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi alisema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa, ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea maghala ya kuhifadhia mahindi ya Nfra yaliyopo Manispaa ya Sumbawanga.

Waziri Zambi alisema kuwa soko la ununuzi wa mazao la  Nfra limemlenga  zaidi mkulima hivyo basi imefika wakati kwamba lazima aweze kunufaika na soko hilo, hivyo ni vema wakulima wakapewa kipaumbele kwenye ununuzi huo wa mahindi badala ya wafanyabiashara ambao wana uwezo wa kusafirisha bidhaa popote lilipo soko la uhakika na kuuza mazao yao.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akizungumza jambo mara alipotembelea ofisi za NFRA mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

"Naiagiza NFRA kuacha mara moja kununua mahindi kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwa wao wanajiweza kiuchumi na wanaweze kwenda kutafuta soko kokote kule lilipo....tuwape kipaumbele wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika na na vile vya akiba na mikopo (Saccos)" alisema Zambi.

Alisema kuwa wafanyabiashara wanapaswa kuwaachia wakulima wadogo na wakati soko la Nfra kwa kuwa hivi sasa serikali ikiangaika kuwatafutia soko la uhakika la mahindi nje ya nchi hususani katika za Kenya, Sudani ya kusini na nchi za kiarabu kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza kipato cha wakulima na kuweza kuondokana na umasikini.
Viongozi wa Serikali mkoa wa Rukwa wakiwa wameongozana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi alipotembelea ofisi za NFRA mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kwa upande wake. Meneja wa mamlaka ya hifadhi ya chakula kanda ya Sumbawanga, Amos Mtafya alisema kuwa msimu huu wa ununuzi wamepangiwa kununua tani 40,000 katika mikoa yote miwili ya Rukwa na Katavi.

No comments