Breaking News

Watatu mbaroni kwa madai ya kuhusika na mauaji ya kaka yao

Watu watatu wanashikiliwa na Polisi mkoani Katavi  kwa wakidaiwa  kuua ndugu zao  katika matukio tofauti  wakiwemo ndugu wawili  wanaodaiwa kumchalanga mapanga kaka yao  mkoani Mwanza .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari   amewataja ndugu wawili , Peter Sangija ‘Ng’umbi”  na  Madukwa Sangija ‘Ng’umbi wakazi  wa kijiji cha Ihushi , kata ya Kisesa  wilayani Magu  mkoani Mwanza
Kwa mujibu  wa Kamanda Kidavashari  watuhumiwa hao  wanadaiwa kumuua ndugu yao  aliyetambuliwa  kuwa Mtaalamu Bahati “Ngu’mbi (55) , Julai 26 , mwaka huu  kwamba mara  baada ya kutenda uhalifu huo walikimbilia kusikojuliakana  hadi  walipokamtwa  mkoani Katavi .

Mtuhumiwa wa kwanza Peter alikamatwa August 25, mwaka huu  saa  sita mchana  kijijini Mtisi  wilayani Mlele ambapo  nduguye aitwaye Madukwa alikamatwa Agosti  26, mwaka  huu akiwa amejificha kijijini Ilembo wilayani  hapa .

Kidavashauri  amedai kuwa  watuhumiwa  hao wanashilikiliwa na Jeshi la Polisi  mkoani hapa  wakisubiri  kurejeshwa mkoani Mwanza kujibu tuhuma zao
.
Katika tukio  lingine kwa mujibu wa Kidavashari , Jeshi la Polisi mkoani hapa  linamshikilia John Mussa (50) akituhumiwa  kumuua  dada yake  aitwae Ester Mussa (47)  wakigombea  shamba la urithi .

Kwa mujibu  wa kamanda Kidavashari  mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 26, mwaka huu  saa mbili usiku kijijini Mnyagala  wilayani Mlele .

Indaiwa kuwa marehemu anadaiwa kumlalamikia kila wakati  mtuhumiwa kwa kuuza  mashamba  yote ya urithi walioachiwa na mrehemu wazazi  wao ambapo  mtuhumiwa alisikika  mara  kwa mara  mitaani  akidai kuwa atakodi  watu  kumuua  dada yake  kwa kumkata kata kwa mapanga .

Kamnda Kidavashari  anadai kuwa  usiku  wa tukio , marehemu akiwa anatoka kwenye shughuli zake  za kika siku  za kuuza mgahawa  akiwa njiani kurejea  nyumbani kwake  alikutana na kaka yake  ambaye alimshambulia kwa kumkata kata kwa  mapanga  kisha akakimbia .

“Jeshi  la Polisi  lilifanikiwa  kumakamata  mtuhumiwa  kwamba atafikishwa  mahakamani  mara  baada  ya uuchunguzi wa  awali kukamilika “ anadai Kamanda

No comments