Breaking News

Auawa kwa kukatwa na mapanga, mwili watupwa ndani ya Ngalawa.

Na Walter Nguluchuma, Katavi.
MTU mmoja ambaye ni mvuvi wa samaki  aliyefahamika kwa jina la   Credo  Amando maarufu kwa jina la Kamanyola (58) mkazi wa  Kijiji cha Majomoto   wilaya ya Mlele Mkoani Katavi, ameuawa baada ya kupigwa kwa kukatwa na shoka kichwani na mwili wake kutupwa Ngarawa mtoni.
Kwa mujibu  ya taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio hilo lilitokea hapo Agosti  29 mwaka huu saa  nyakati za usiku kijijini hapo

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu aliondoka  nyumbani kwake  nyakati za saa tatu asubuhi na kuelekea kwenye shughuli zake za kila  siku  za  uvuvi wa samaki kwenye mto  Kavuu ulipo kwenye Kijiji hicho cha Majimoto na hakuweza kuonekana tena.
Inadaiwa kuwa wavuvi wenzake waliokuwa wamefika kwenye eneo hilo kwa lengo  kuvua samaki waliona Ngarawa pembezoni mwa mtohuku ndani yake  kukiwa na mwili wa mtu.

Alisema wavuvi hao waliamua  kwenda ilipokuwepo Ngarawa hiyo  na ndipo  walipoweza  kuuona mwili wa marehemu Credo  ukiwa ndani ya Ngarawa pembezoni mwa mto  Kavuu huku marehemu akiwa  na majeraha makubwa  sehemu mbalimbali za mwili wake

 Wavuvi hao  walikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao nao walitoa taarifa kwenye  kituo cha Polisi cha Maji moto ambao walifika kwenye eneo hilo na kisha mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na kubaini  kifo hicho kilitokana na marehemu kupingwa na kitu kizito kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake

Kamanda Kidavashari alisema  katika tukio  hilo hakuna mtu wala watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo hivyo kabla ya kutokea kifo hicho  marehemu alikuwa akikorofishana na watu mbalimbali  Kijijni hapo kutokana na tabia yake ya ulevi  uliokithiri wa unywaji wa pombe
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili wahusika au muhusika aweze kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheriaili iweze kuchukua  mkondo wake

No comments