Wananchi Rukwa, watahadharishwa kuhusu homa ya Ebola
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya |
Mhandisi Manyanya ametoa tahadhari jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kuhusu hatua ambazo serikali imechukua kuhakikisha ugonjwa huo haupati nafasi ya kuingia nchini baada ya kuripotiwa kuingia katika katika taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kusababisha vifo vya watu kadhaa.
Alisema kuwa ni vema wananchi wakachukua tahadhari na kuanza kujikinga na maradhi hayo kwa kuwa ugonjwa huo ulioripotiwa kuingia DRC ambayo inapakana na mkoa wa Rukwa na kumekuwa na mwingiliano mkubwa watu wanaingia nchini kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kibiashara na uvuvi katika ziwa Tanganyika.
Manyanya alisema kuwa mkoa huo tayari umepokea vifaa maalum kutoka wizara ya afya ambavyo vitatumika kwa ajili ya kinga vimewasili.
Aliongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi hasa waishio maeneo ya mipakani kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo unaoenezwa kwa kula nyama za nguluwe weusi, sokwe, swala nyani na popo.
Aliwataka wananchi kuacha kutumia vitoweo hivyo kwa kuwa wanaweza kuambua maambukizi ya virusi vya homa ambavyo upenda kujificha kwenye wanyama hao.
Pia aliiomba wizara ya afya kuwapatia
vifaa vya kupima joto kwa kuwa kuna umuhimu wa vifaa hivyo ili waweze
kupima mgonjwa anayeingia kabla ya kufika mbali zaidi hivyo kuna umuhimu
mkubwa wa kuwa na vifaa hivyo kwa kuzingatia kwamba mkoa huo upo
mpakani na unapakana na DRC.
No comments