Breaking News

KIWALI: NALITAKA JIMBO LA KALAMBO KWA KUWA LIMEKOSA UWAKILISHI SAHIHI

Richard Kiwali (37)
KIPENGA cha uchaguzi hakijapulizwa, lakini tayari wanasiasa wamevaa jezi kitambo wakipiga jalamba katika majimbo mbalimbali. Hofu ni kwamba, wasije wakamaliza pumzi kabla ya mchezo kuanza.

Naam. Ni mwaka mwingine wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, ambao, kama chaguzi nyingine zilizopita, unabashiriwa kuwa na changamoto nyingi, ingawa za safari hii zinaweza kuwa kubwa zaidi.

Ukubwa wa changamoto hizi unatokana na mageuzi kushika kasi, huku vijana wengi wakijitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba 2014.

Vuguvugu la mageuzi liko hadi vijijini na  kwa hakika vijana wengi wameonekana kuguswa na kutamani kushika nafasi za uongozi licha ya taaluma zao walizonazo.

Jimbo la Kalambo mkoani Rukwa ni miongoni mwa majimbo mengi yanayotajwa kutokuwa na maendeleo licha ya fursa nyingi zilizopo, na ambayo wabunge wake wanaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutokana na wimbi hilo la vijana wanamageuzi.

Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Kandege Josephat Kandege (CCM), tayari anaonekana kupata mpinzani baada ya kujitokeza kwa kijana Richard Kiwali (37), msomi ambaye anaamini kudumaa kwa maendeleo jimboni humo kumetokana na 'kujisahau' kwa wabunge waliopo na waliopita na kuwaacha wananchi wakiendelea kuogelea kwenye lindi la umaskini.

Kiwali, ambaye ana shahada ya Maendeleo ya Jamii, anasema ameamua kutangaza nia kuwania jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako uhuru wa maoni unaonekana kupewa kipaumbele tofauti na CCM.

"Jimbo hili limekosa uwakilishi sahihi kwa 
maana ya kuyachukua matatizo ya wananchi kutoka kwenye maeneo yao na kuyafikisha kwenye vyombo mbalimbali vya maamuzi
​ a
mbavyo vingeweza kuwa chachu ya kutatua matatizo hayo, wananchi wanakabiliwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi lakini hakuna mtu wa kuwasaidia kufanya hivyo
​," anasema Kiwali​
.

K

​i​
wa
​li​
​anasema ili kufikia lengo hilo ni wakati sasa wa 
kufanya mabadiliko
​ili
kupata uwakilishi sahihi utakaosukuma gurudumu la maendeleo lililokwama
​ jimboni humo ambamo kuna fursa nyingi lakini zimeshindwa kusimamiwa na kuibuliwa ipasavyo​
.

S

​uala la​ ajira na uchumi ni s
ababu nyingine
​ambayo Kiwali anasema inaweza kutatuliwa kwa kuweka mikakati madhubuti na inayotekeleza, kwani ​
asilimia kubwa ya wananchi wa
​ jimbo hilo 
ni wazalishaji katika sekta ya kilimo,
ambayo
​ 
ndi
​y​
o shughuli 
wana
​yo​
itegemea kwa ajili ya kipato chao cha kila siku.

​"Tungekuwa 
na kilimo bora
​tungeweza kuongeza 
ajira kwa vijana
​ambao wangejihakikishia 
mazingira mazuri ya maisha
​badala ya
kufikiria kukimbilia mijini.
​ ​Pembejeo zikija kwa wakati zingewasaidia wakulima kutekeleza vyema shughuli za kilimo, lakini sasa pembejeo hizo zinaletwa miezi miwili baadaye, tena wakati msimu wa kupanda umepita," anasema.

​Vile vile, Kiwali anazungumzia shughuli za u
vuvi katika mwambao wa
​Z
iwa Tanganyika,
​ akibainisha kwamba shughuli hizo zimekuwa hazina tija kwa jamii kutokana na kukosekana kwa zana bora​, masoko ya uhakika na mfumo mzuri wa uuzaji wa samaki na mazao mengine ya ziwani, ikiwa ni pamoja na elimu ya uvuvi bora na endelevu kwa wananchi
.
​ "Ziwa Tanganyika lina samaki wengi, lakini wavuv​i wanashindwa kufikia malengo kwa sababu kwanza hawana elimu bora ya shughuli wanazozifanya, hawana zana za kisasa na zaidi hakuna masoko ya uhakika, wanawezaje kujikwamua kiuchumi ikiwa kero hizi hazikutatuliwa," anasema Kiwali na kuongeza kwamba sekta hiyo ikiendelezwa na kujengewa mazingira mazuri inaweza kukuza kipato cha familia na kuinua uchumi wa taifa kwa ujumla.

​ Suala la uwekezaji katika jimbo hilo nalo ni changamoto kubwa licha ya kuwepo kwa maeneo mengi mazuri yanayofaa kwa kilimo, lakini uwekezaji katika sekta ya utalii pia ni duni ingawa Maporomoko ya Kalambo yapo jimboni humo lakini hayawanufaishi wananchi.

"Maporomoko ya Kalambo ni kivutio kikubwa cha utalii, uwe wa ndani au wa nje, lakini ingawa maporomoko haya yapo kwetu Tanzania, hayawanufaishi wananchi badala yake wenzetu Wazambia wanayatumia kuingiza fedha za kigeni.

"Pale Kasanga ni eneo la kihistoria kwani kulikuwa ngome ya Wajerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Pakiendelezwa pale panaweza kuliingizia taifa fedha nyingi, na kazi ya kwanza ni kuyatangaza maeneo haya na kuweka mandhari nzuri ili kuwavutia watalii," anafafanua.

​Kiwali anasema endapo atachaguliwa, 
vipaumbele
​vyake vikubwa ni ​
vinne vikubwa,
​ambavyo 
ni
​el
imu,
​a
fya,
​k
ilimo na
​m
iundombinu.
​ "Pamoja na kuwepo kwa hamasa kubwa​ katika uandikishaji wa wanafunzi, lakini ni wachache wanaofanikiwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari. Hapa kuna tatizo."

​ "Utoro, mimba na mwamko duni wa kielimu kwa wazazi ni sababu tu zinazofanya watoto wengi washindwe​ kuhitimu, hivyo ni lazima, kama mwakilishi, kuhakikisha wananchi wanaelimishwa umuhimu wa kuwasomesha watoto, hasa wa kike, ambao mara nyingi ndio wanakuwa wahanga wa kutomaliza elimu ya msingi na sekondari," anasema na kuongeza kwamba ataisimamia serikali kuhakikisha inatatua changamoto za uhaba wa vitabu na maabara na kuyafanya mazingira ya shule yawe rafiki kwa wanafunzi.

​Kuhusu 
​changamoto 
​ ya afya, anasema jimbo hilo liko nyuma katika sekta hiyo kwani hakuna zahanati wa vituo vya afya​ vya kutosha na hata vile vilivyopo vinakabiliwa na uhaba wa dawa. "Wagonjwa wakifika wanaishia kupimwa tu, dawa wanaambiwa wakanunue. Kuna wazee na watoto, na hali ya maisha ya vijijini inafahamika, watapata wapi fedha hizi za kununulia dawa?"

​ Uhaba wa maji safi na salama ni changamoto nyingine kubwa jimboni humo, ambapo Kiwali anasema, wananchi wanalazimika kunywa maji yanayotumiwa na mifugo na wanyamapori.

​ Kiwali anaongeza kwamba, sekta ya kilimo iko nyuma kimaendeleo jimboni humo kutokana na kukosekana kwa pembejeo kwa wakati na pia ukosefu wa masoko ya uhakika ili kukifanya kilimo kiwe na tija kwa wakulima
.

​ "Wakulima wanakopwa mazao yao kutokana na kukosekana kwa masoko ya uhakika, lakini tatizo la miundombinu bora, hasa ya barabara nalo linachangia kurudisha nyuma maendeleo katika jimbo hili," anasema Kiwali.

​Kiwali, aliyezaliwa 
mwaka 1978,
​k​
atika
​K
ijiji cha Mwazye
​,​
​W
ilaya ya Kalambo mkoa
​ni
 Rukwa,
​alipata e​limu ya msingi katika shule ya
​ 
Mwazye,
​akaenda ​
Sekondari
​ya ​
Kaengesa
​na kumalizia katika 
Seminari
​K
uu
​ya ​
Peramiho mkoa
​ni 
Ruvuma kwa masomo Falsafa
​ na
Th
​e
oloji
​a​
​na baadaye mwaka 2011 alipata ​
Shahada ya Ustawi wa Jamii katika taasisi ya ustawi wa jamii jijini Dar es salaam.

No comments