Breaking News

MATUKIO YA HABARI ZA VIJIJINI KATIKA PICHA

Msichana mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake akichota maji kwa taabu jana katika moja kisima katika kijiji Malagano kilichpo nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo la ukosefu huduma ya maji safi kutokana na kutokuwa na miundombinu  ya maji.

Wasichana wawili wakazi wa kijiji cha Kankwale mjini Sumbawanga mkoani Rukwa akiwa wamebeba mzigo wa kuni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama alivyokutwa jana na mpiga picha wetu.
Mzee Amos Kissy mkazi wa kijiji cha Milanzi ambaye ni msanii wa kikundi cha Asili cha Chatakwa akipuliza vuvuzela la asili jana wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM ambapo mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilaly aliwahutubia wananchi wa kata hiyo.
   

No comments