MWALIMU AUAWA KWA KUCHOMWA NA VISU MPANDA
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwita Paulo (Ryoba)
25 mwalimu wa Shule ya Msingi Lukama Makazi ya Wakimbizi ya Katumba
Mkoa wa Katavi ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na visu kifuani na
watu wasiojulikana
Tukio la mauaji hayo ya kikatili dhidi ya mwalimu huyo
lilitokea hapo juzi majira saa mbili usiku katika eneo la shule ya
msingi Mpanda katika mtaa wa Mpanda Hotel mjini hapa
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa marehemu kabla ya
kifo chake hicho aliaga kwenye kituo chake cha kazi katika shule ya
Msingi Lukama kuwa anakwenda mjini Mpanda katika shule ya Sekondari ya
Mwangaza kufanya mtihani wa kidato cha sita
Alisema marehemu alikuwa amefuatana na waalimu wenzake
ambao wanafundisha shule za msingi mbalimbali zilizoko kwenye makazi
hayo ya Wakimbizi ya Katumba ambao nao walikuwa wanakwenda kufanya
mtihani wa kidato cha sita kwenye kituo cha kufanyia mtihani katika
shule ya Sekondari ya Mwangaza
Kidavashari alieleza marehemu akiwa na waalimu hao
aliweza kufika katika shule ya mwangaza na kufanya mitihani yake
ambapo alikuwa akirudia kufanya mtihani ya baadhi ya masomo ambayo
hakuwa amefanya vizuri katika masomo yake ya kumaliza kidato cha sita
Baada ya kumaliza mitihani walimu huyo na wenzake
walianza safari la kurejea kwenye vituo vyao vya kazi katika makazi ya
wakimbizi ya Katumba lakini yeye aliamua kubaki mjini Mpanda
Alisema baada ya hapo marehemu Paulo hakuonekana tena
mpaka mwili wake ulipoonekana katika eneo la shule ya Msinngi
Mpanda mtaa wa Mpanda Hotel huku ukiwa amechomwa visu katika
sehemu zake za kifuani
No comments