Breaking News

MBUNGE AESHI AMWAGA MISAADA KWA WAHANGA WA MAAFA YA KIMBUNGA S'WANGA

 KAYA 30 ambazo zilibomolewa makazi yao na kimbunga katika kijiji cha Katumba Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa huenda wakapata ahueni ya maisha baada ya kupewa misaada mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Aeshi Hilary jana alikabidhi misaada hiyo ikiwemo ni pamoja na magodoro 30,unga wa ugali sabuni na vitu vingine ili viwasaidie watu waliopata maafa yaliyotokea April 12 baada ya mvua kubwa kunyesha kijijini hapo.

Akikabidhi misaada yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 3, Hilary alisema kuwa yeye ndiyo mbunge wao na hivyo anawajibika moja kwa moja na matatizo yao hivyo ameona ni vema kuanza kuwapa unga wa ugali kwaajili ya chakula pamoja na magodoro ili waweze kulala vizuri wakati misaada mingine inatafutwa.

‘’mimi ni Mbunge wenu….ninawajibika moja kwa moja na matatizo yenu,hivyo basi nimejitahidi nimepata hiki kidogo nilichowaletea leo, naomba mkipokee na bado tutajitahidi kadiri ya kudra za Mwenyezi Mungu kuhakikisha mnarejea katika hali yenu ya kawaida’’…alisema.

Mbunge Aesh pia alitoa fedha kiasi cha Sh milioni 5,000,000 katika kijiji cha Mlanda kwaajili ya ujenzi wa josho la kuoshea mifugo kijijini hapo fedha ambazo zilikuwa ni ahadi yake wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani aliwaahidi wananchi hao angewapa kutatua tatizo hilo la ukosefu wa josho.

Mmoja wa wahanga ambaye nyumba yake ilibomoka kabisa Alistid Mavunje alisema kuwa msaada wa mbunge huyo umetolewa wakati muafaka kwani baadhi ya familia zilikuwa zikikabiliwa na njaa kutokana na kuharibika kwa vyakula.
Alisema baadhi ya familia zilikuwa zikihangaika hata sehemu ya kulala hasa wakina mama na watoto wadogo licha ya kuwa walipewa hifadhi na wanakijiji wenzao lakini walikuwa wakikabiliwa na tatizo la magodoro pamoja na mikeka ya kulalia.

‘’kuna baadhi ya akina mama walikuwa wakilala chini na watoto wao…nahii hali ya baridi kali tulianza kuhofu tungepoteza watoto wadogo kwa ugonjwa wa nimonia kutokana na kutolala pazuri lakini pia tunaomba akipatikana mtu wa kutoa mablanketi atusaidie maana bado hilo ni tatizo’’…..alisema Mavunje.
Awali, Mwenyekiti wa CCM Sumbawanga mjini, Selemani Kilundi  alisisitiza kuwa wawe wavumilivu katika wakati huu mgumu yeye binafsi pamoja na serikali watahakikisha wananchi hao wanatatuliwa kero zinazo wakabiri haraka iwezekanavyo ili waendelee na shughuli zao za uzalishaji mali.

Kaya zaidi  ya 30  katika  kijiji cha Katumba, nje kidogo ya Manispaa  ya Sumbawanga mkoani Rukwa  mwezi uliopita zilipata maafa baada  ya  nyumba zao  kuezuliwa paa  na zingine  kubomoka kabisa  kufuatia  mvua  kubwa iliyoambana na upepo  mkali iliyonyesha juzi .

No comments