POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA MADEREVA BAJAJI WALIOANDAMANA S'WANGA LEO.
ENEO la Soko kuu mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo mchana liligeuka kuwa uwanja wa mapambano baina ya askari polisi na
madereva wa pikipiki za magurudumu matatu’bajaj’ kugoma na
kufunga barabara kwa kulala kifudi fudi.
Kitendo hicho kilisababisha kusiamama kwa huduma ya usafiri katika
barabara kuu inayounganisha mji ya Sumbawanga na Tunduma kwa
saa kadhaa na kusababusha askari polisi kufyatua risasi
hewani na kurusha mabovu ya machozi ili kuwatawanya .
Askari wa kuliza ghasia (FFU)walifika eneo hilo la tukio wakiwa na
silaha nzito wakitumia usafiri wa gari lao lenye namba PT
1854 tayari kukabiliana na mgomo huo .
Licha ya madereva hao kulala kifudifudi barabarani pia waliweka
mbao zilizopigiliwa misumuri kuzuia gari lolote lisipitie
eneo hilo la tukio na kuchoma matari ya magari .
Shughuli za kawaida katika soko kuu la mjini Sumbawanga zilisimama kwa muda wa
saa moja baada ya jeshi la polisi mjini hapo kuvutana juu ya mgomo wa ghafla
ulioitishwa na madereva wa pikipiki za magurudumu matatu maarufu kwa jina la
bajaji.
Kaimu Kamanda Polisi mkoa wa Rukwa, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Leons
Rwegasira amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kueleza kuwa bado jeshi hilo
linatumia busara kulishughulikia tatizo hilo kabla ya kuanza kamata
kamata.
Aliongeza kuwa hakuna majeruhi aliyeripotiwa wala uharibifu wowote uliotokana
na vurugu hizo ambapo aliwasihi vijana kuacha kujichulia sheria mkononi na
kuanza kurusha mawe kwenye gari la polisi.
Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa moja zimetokea leo
saa sita mchana ambapo madereva hao wa bajaj wanaaotoa
huduma za usafiri katika Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake
vilisababisha taharuki kubwa kwa wakazi wa mjini humo.
Mwenyekiti wa madereva hao, Fred Jackson alisema wameamua kugoma kutokana na
utaratibu wanaoutumia askari wa usalama barabarani mjini Sumbawanga ambapo kila
siku wamekuwa wakipanga kiwango cha makusanyo ya fedha kutoka kwao na hivyo
kulazimisha makosa yasiyokuwapo.
Alisema wameshajipanga kugoma mpaka uongozi wa serikali utakapoyashughulikia
malalamiko yao ikiwa ni pamoja na kuwabaini askari wa usalama barabarani
wanaofanya ukamataji kwa lengo la kujipatia kipato na siyo kusimamia sheria.
No comments