MWALIMU MSTAAFU JELA MAISHA KWA HATIA YA KUMBAKA MJIKUU WAKE
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu
mwalimu mstaafu wa Shule ya Msingi Mpanda Ndogo Wilayaya ya Mpanda Rashid
Mbogo kifungo cha maisha jela
baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka
mjukuu wake (5) na kumuharibu vibaya
sehemu zake za siri
Hukumu hiyo ilisomwa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pande zote
mbili za mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Godfrey Rwezabila alidai mahakamani kuwa mshitakiwa Rashid Mbogo alitenda kosa hilo oktoba 19 mwaka jana majira ya saa mbili na nusu usiku nyumbani kwake huko katika Kijiji cha majalila Wilayani hapa
Siku hiyo ya
tukio mshitakiwa alidaiwa kumbaka mjuu kuu wake huyo wakati akiwa amelala chumbani kwenye godoro wakati akiwa amelala na mtoto wake na Rashid Mbogo aitwaye Faraji
Mbogo(9) ambae alishuhudia
wakati baba yake akimbaka mtoto huyo
Ilielezwa mahakamani na mwendesha mashitaka
kuwa siku hiyo mke wa mshitakiwa alimuuga
mume wake kuwa anakwenda kwenye zizi la mbuzi lililokuwa jirani na nyumbani kwao
kufungia mbuzi ndipo alipotumia nafasi
hiyo ya kuingia chumbani na kumkuta mjuu kuu wake akiwa amelala na mtoto
wake na kisha alimshika na kuanza kumbaka
huku mtoto wake wa kuzaa mwenyewe akiwa anashudia tendo hilo
Alieleza
mshitakiwa aliweza kukamatwa siku hiyo hiyo na majirani zake ambao walimpeleka hadi kituo cha polisi cha
Wilaya ya Mpanda huku mjukuu wake nae alikimbizwa kwenye hospitali ya Wilaya ya
Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa matibabu
baada ya kuwa ameharibiwa vibaya kwenye sehemu zake za siri
Mshitakiwa katika
utetezi wake ambapo hakuna na
shahidi hata mmoja huku upande wa mashitaka ukiwa na mashahidi
sita akiwepo mtoto wake mwenyewe Faraji
Mbogo alikana kutenda kosa hilo kabisa kwalealicodai mahakamani hapo kuwa umri wake ni mkubwa na kwa sasa
ameishaishiwa nguvu za kiume hivyo asingetenda kosa hilo
Baada ya utetezi
huu mahakama iliamuru mshitakiwa akapimwe hospitalini ili baini kama kweli hana nguvu za kiume ambapo majibu ya daktari
yalionyesha kuwa Rashid Mbogo bado
anazo mbegu za kiume zinazomfanya atende tendo la ndoa
Hakimu Chiganga
baada ya kurudhika na ushahidi
uliotolewa aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na kosa la kifungu cha sheria
namba 130 na 131 cha marekebisho
ya sheria ya mwaka 2009
Akisoma hukumu
hiyo alisema kutokana na kuapatikana na kosa hilo bila mashaka yoyote mahakama imemuhukumu
Rashid Mbogo kutumikia kifungo
cha maisha jela kuanzia jana.
No comments