WASWIDENI WAWATUNUKU TUZO WAANDISHI RUKWA.
Na Mwandishi wetu,
Sumbawanga.
WAANDISHI wa habari watano wa mkoa wa Rukwa, wakiongozwa na Mhariri wa blog ya Pembezonikabisa wametunukiwa tuzo kwa kuwa na mchango mkubwa katika kuandika na kutangaza habari za afya na ujinsia.
Sumbawanga.
WAANDISHI wa habari watano wa mkoa wa Rukwa, wakiongozwa na Mhariri wa blog ya Pembezonikabisa wametunukiwa tuzo kwa kuwa na mchango mkubwa katika kuandika na kutangaza habari za afya na ujinsia.
Mhariri wa blog ya Pembezonikabisa, Mussa Mwangoka akipokea tuzo yake. |
Waandishi hao wa habari ni Mussa Mwangoka ambaye licha ya kuwa mhariri wa mtandao huu pia ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peti Siyame (Habarileo/Daily News), Joshua Joel (ITV), Nswima Ernest (TBC) na Juddy Ngonyanya kutoka Channel ten.
Mratibu msaidizi Shirika la Afya ya Uzazi la Sweden (RFSU), Eugenia Msasanuri,
alisema kuwa waandishi hao wa habari walikuwa mstari wa mbele kuandika
na kutangaza habari za Afya na Ujinsia kupitia mradi wa wa
ushirikishwaji wanaume Tanzania katika haki ya uzazi, afya na ujinsia(TMEP) ulikuwa ukitekelezwa katika mikoa miwili hapa nchini ya Rukwa na Singida.
Waandishi wakiwa wameshika tuzo walizotunukiwa na RFSU, hapo katika picha ya Pamoja na mlezi wa klabu ya waandishi ya Rukwa, Mkuu wa wilaya ya Nkasi Iddy Kimanta aliyeketi katikati. |
Alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, RFSU ilikuwa ikishirikiana na shirikali lisilo la kiserikali la Resource Oriented Development Initiative (RODI) kwa Rukwa na Health Action Promotion Association (HAPA) kwa upande wa Singida.
Tuzo
hizo zilikwenda sambamba na kukabidhiwa vyeti ikiwa ni ishara ya
kutambua na kuthamini mchango wao katika kuripoti taarifa hizo lengo
likiwa ni la kuleta ushiriki sawa wanaume kwenye afya ya uzazi ambapo
imesaidia kuhamasisha wanaume kuambatana na wake zao kliniki kabla,
wakati
na baada ya kujifingua lakini pia kufanya kuwepo na ushiriki wa moja kwa
moja katika masuala ya uzazi na malezi ya familia.
Akikabidhi zawadi hizo, Afisa tawala wa mkoa wa Rukwa, Erasmus Rugarabamu baada ya kukabidhi tuzo hizo, aliwapongeza waandishi hao wa habari
na kuongeza kuwa kuondoka kwa wafadhili kusiwe sababu ya kufa kwa mradi
huo halmashauri husika zinapaswa kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu
kwa manufaa ya jamii.
Kwaupande wake, Peti Siyame
ambaye pia Mwenyekiti wa Klabu wa waandishi wa habari ya Rukwa, alisema
waandishi hao wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na weledi na sio tuzo
walipata ziwafanye wabweteke na kusahau majukumu yao mbele ya jamii.
No comments