Mwandishi RTD afariki dunia dunia na kuzikwa Katavi
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Mwandishi wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) kabla ya kuwa shirika la Utangazaji (TBC) hivi sasa Lucas Matipa (77) amefariki Dunia na kuzikwa huko wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Padri Somoni Matipa alisema Lucas alifariki hapo jana jioni nyakati za saa 12:30 nyumbani kwao maeneo ya mtaa wa Majengo Manispaa ya Mpanda.
Padri Matipa alisema marehemu alizaliwa mwaka 1940 huko katika Tarafa ya Karema wilaya ya Mpanda ambayo kwa sasa ni wilaya ya Tanganyika na alistaafu kazi ya uandishi wa Habari na utangazaji wa RadioTanzania mwaka 2006.
Inaelezwa kwamba enzi za uhai wake alifanya kazi kama mwandishi wa habari na mtangazaji wa RTD ambapo miongoni mwa aliofanya nao kazi ni marehemu David Wakati.
Alisema marehemu Lucas Matipa alianza kusumbuliwa na maradhi tangu mwaka juzi hali ambayo ilimlazimu atoke Dar es salaam alikokuwa akiishi na kurudi nyumbani kwao Mpanda.
Ibada ya maziko ilifanyika jana katika kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda na ibada hiyo iliongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo Padri Dominick Odiyambo aliyesaidiana na Padri Simoni Matipa.
Wakati wa misa hiyo ya mazishi Padri Odyambo alieleza kuwa marehemu Lucas Matipa wakati wa uhai wake alifanya kazi vizuri ya uandishi wa habari na utangazaji vizuri .
Alisema kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi ya uandishi wa habari ndio maana taifa lilimwamini na yeye alibahatika kuzungumza nae mara kwa mara katika kipindi cha hivi karibuni na alikuwa akimwelezea jinsi alivyofanya kazi ya uhandishi wa habati hapa nchini na nje ya nchi kabla ya kustaafu kwake 2006.
Mazishi ya marehemu Lucas Matipa yalifanyika jana katika makaburi ya Mwangaza na yalihudhuliwa na mamai ya wakazi mji wa Mpanda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
No comments