Breaking News

Wanahabari wapigwa msasa kuhusu Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala bora



Mwandishi wa habari wa gazeti la Zanzibar Leo ( Zanzibar), Mwinyimvua Abdi Nzukwi akichangia mada katika mafunzo ya siku tano ya Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala bora yanayofanyika katika hotel ya Flomi mjini Morogoro na kuratibiwa Umoja wa KLabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)

Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu, Demokrasia na Utawala bora, Wakili Juma Thomas akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari kutoka mkoa mbalimbali nchini, mafunzo hayo yanaratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi Tanzania (UTPC)

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Haki za binadamu, Demokrasia na Utawala bora yanayofanyika katika hotel ya Flomi Mjini Morogoro, kutoka kushoto ni Tunu Herman (Majira - Mwanza) , Samweli Mwanga (Mtanzania - Simiyu) na Mussa Mwangoka (Pembezoni blog - Rukwa).
Wanahabari wengine, wakifuatilia mafunzo kutoka kushoto ni Asha Athumani (Mbeya) na Rhoda Ezekiel wa gazeti la Uhuru kutoka mkoa wa Kigoma.










No comments