Breaking News

Mvua yaleta madhara Sumbawanga.



Na Mwandishi wetu, Rukwa.

Mvua kubwa iliyonyesha mfulululizo kwa zaidi ya saa tatu imesababisha madhara kwa wakazi wa eneo la Jangwani mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, ikiwemo baadhi ya nyumba kukumbwa na mafuriko.



Mvua hiyo iliyoanza kunyesha nyakati za saa saba mchana na kukatika saa 10 jioni, imesababisha maji kujaa katika baadhi ya nyumba hali iliyosababisha usumbufu kwa wamiliki na wanaoishi katika nyumba hizo hali iliyowalazimu kubeba watoto wao na kuyakimbia makazi yao kwa muda.

John Peter alisema haya mafuriko yanasababishwa na mkandarasi aliyejenga barabara ya Mpanda kuelekea Kanisa katoliki kwa kiwango cha lami kuna eneo la makutano na barabara ya Two ways hajaweka mtaro wa kuruhusu maji kwenda upande wa pili wa barabara hiyo.

Alisema kilio hicho ni cha muda mrefu sasa lakini licha ya kueleza tatizo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na kwa mkandarasi wa barabara hiyo  lakini  hakuna hatua zilizochukuliwa.

Aliomba uongozi wa halmashauri hiyo kuona uwezekano wa kutatua changamoto hiyo kwa kuwa hiki ndio kipindi ambacho mvua nyingi zinaendelea kunyesha.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema hadi sasa hajapokea taarifa ya vifo wala majeruhi kufuatia mvua hiyo.


No comments