Breaking News

RC Rukwa ataka barabara ya Sumbawanga - Kasanga iishe haraka

Mhandisi wa Tanroads mkoa wa Rukwa, Suzan Lucas akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Sumbawanga kuelekea bandari ya Kasanga juzi.
Na Mwandishi wetu, Rukwa.

Uongozi wa Serikali mkoani Rukwa umeitaka Wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi kumlipa fadha zaidi ya bilioni 12 mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya  Sumbawanga hadi bandari ya Kasanga ili aweze kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo haraka iwezekanavyo.


Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachimu Wangabo alisema mara baada ya kutembelea barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 112 inayojengwa na mkandarasi kampuni ya Joint Venture of railway 15G/ New Centry Company LTD kutoka nchini katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo umechukua muda mrefu sana ambapo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2010 na ulipaswa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu lakini hadi sasa haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni mkandarasi kutolipwa fedha zake kwa wakati.
Alisema kutokana na hali hiyo inafanya gharama za utekelezaji wa mradi kuwa kuwa na thamani ya mradi huo kutoonekana, hivyo upo umuhimu wa wizara hiyo kufatua fedha na kumlipa mkandarasi huyo ili ujenzi wa barabara hiyo kukamilike haraka iwezekanavyo.

"Barabara hii ina manufaa sana kwa maendeleo ya kiuchumi wa mkoa huu kwa kuwa ikikamilika itawezesha kuanza kutumika kwa bandari ya Kasanga ambapo itasaidia kuboresha mawasiliano baina ya nchi jirani za KongoDRC, Burundi na Zambia ambazo zitaitumia bandari hiyo kwa ajili kusafirisha mizigo yao kupitia Ziwa Tanganyika.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo sio tu kuongeza ajira rasmi na zisizo rasmi kupitia bandari ya Kasanga, lakini mapato ya serikali na kukuza uchumi wa mkoa na mtu mmoja mmoja.

Awali, kaimu meneja wa Wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Rukwa, Jotrevas August alisema kuwa mradi wa upembuzi yakinifu na ujenzi wa barabara hiyo ulianza tangu januari 2010 na umegharimu Sh bilioni 133.

Alisema kuwa licha ya serikali kuchelewa kutoa fedha kw ajili ya utekeleza wa mradi ambao umekamilika kwa asilimia 72, pia kumekuwepo na changamoto kadhaa ikiwemo ya kuwepo kwa maeneo mengi yenye maji na mwinuko na mitelemko mikali imechangia kucheleweza kukamilika kwa kazi hiyo.

No comments