Breaking News

Kukimbilia kwa waganga wa kienyeji sio suluhu la matatizo ya uzazi

WANAWAKE wametakiwa kuacha dhana iliyojengeka miongoni mwao kuwa waganga wa jadi ndio suluhu la kutibu maradhi ya kukosa watoto badala yake waende na wanaume zao kwenye Kliniki za afya ili wapate uchunguzi zaidi wa kitabibu na kutatua tatizo hilo.
 Mratibu mradi wa shirika la Swedish Association for Sexuality Education (RFSU) Dk. Cuthbert Mendaenda,alisema hayo wakati akitoa mada kwenye mafunzo ya afya ya uzazi na ujinsia kupitia mradi wa Tanzanian Men as Equal Partners (TMEP)yaliyoshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Singida na Rukwa ambayo yanafanyika katika ukumbi wa Kalenga west Park Hotel uliopo mjini hapa.
Dk. Maendaenda alisema kwamba zipo sababu nyingi zinazochangia wanaume na wanawake kukosa watoto likiwemo suala la mzunguko wa hedhi kwa wanawake hivyo sasa iwapo wote hawafahamu kuhusu jambo hilo ni vugumu kupata suluhu ya tatizo hata wakienda kwa waganga wa kienyeji.

"Wanawake na wanaume hatujazoe kukutana kimwili wakati wa hedhi.....sasa ipotokea yai lipevuka wakati wa hedhi ambao hatujazoea kukutana maana yake ni kwamba hawezi kupata ujauzito jambo ambalo kama hujaenda kuwaona wataalam wa afya ni vigumu kupata kupata suluhu yake" alisema Dk Maendaenda

Pia aliongeza kwamba jamii inapaswa kuondokana na dhana potofu kuwa mwanaume wakifunga uzazi wanapoteza uwezo wa kufanya tendo la ndoa kabisa kitu ambacho kinasababisha wanaume wengi kutokubali kufunga uzazi hivyo kuzaa watoto wengi bila kufuata uzazi wa mpango.
"Tusaidie kuelimisha na jambo hili, wanaume hawataki kufunga uzazi kwa kisingizio cha kupoteza nguvu za kiume.....si kweli ni taarifa ambazo zimejaa upotoshaji mkubwa na hatupaswi kuufumbia macho" alisema.
Kwa upande wake, Meneja mawasiliano wa RFSU, Eugenia Msasanuri alisema kuwa mafunzo hayo kwa wanahabari wa mikoa ya Rukwa na Singida yamelenga kusaidia kutoa elimu kwa jamii ya mikoa hiyo kuhusu ushiriki wa wanaume kwenye masuala ya afya ya uzazi hali ambayo itapunguza mifumo dume ambayo imekuwa ikisababisha ndoa nyingi kuvunjika.
Alisema kuwa jamii ikielimishwa  na wanaume wakashiriki kikamilifu katika afya ya uzazi itasaidia pia kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano hivyo malengo ya Serikali kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 75 ifikapo 2015 yanaweza kufikiwa.

No comments